Saturday, 16 June 2018

Thursday, 8 February 2018

Hivi ndivyo unavyoweza kujua kama una upungufu wa Maji Mwilini

Hivi ndivyo unavyoweza kujua kama una upungufu wa Maji Mwilini

Upungufu wa maji mwilini ni;
Pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

NINI HUSABABISHA?
Sababu zinazosabababisha mwili kukaukiwa maji huweza kuwa nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni pamoja na:

1. Kuacha kunywa maji
2.Kukaa kwenye joto kwa muda mrefu.
3.Kunywa kiwango kikubwa cha pombe
4.Ungonjwa wa kisukari ambao husababisha mtu kukojoa mara kwa mara.
5. Kutokwa na jasho jingi, kwa sababu ya ama kufanya kazi ngumu au mazoezi.
Hivyo inashauriwa mtu anayetokwa jasho jingi kunywa maji mara kwa mara wakati akiendelea na shughuli inayomtoa jasho.

Kama ukiugua au ukipatwa na homa kali, huweza kupungukiwa na maji mwilini
Kutapika na kuharisha nako huweza kupoteza maji mwilini. Hivyo itakeapo hali hiyo jitahidi kunywa maji mwilini.

Hizi ndizo dalili za kukaukiwa na maji mwilini kwa watoto wadogo;
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

Kukojoa mara chache sana

Mtoto kutokuwa mchangamfu

Macho.

Tumbo au mashavu kubonyea 

Mdomo na ulimi kukauka.

Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.

Dadili za upungufu kwa wazee.
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.

Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Vyakula vinavyoondoa mamumivu wakati wa hedhi kwa wanawake

Vyakula vinavyoondoa mamumivu wakati wa hedhi kwa wanawake

Kila mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika, wapo baadhi ya wanawake huumwa na kiuno, wengine tumbo n.k

Dlili za matatitizo ya hedhi
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

Vifatatavyo ni vyakula vinavyoweza kutibu maumivu wakati wa hedhi

2. Tangawizi
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

2. ufuta.
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

3. Papai
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

4. Juisi za mboga za majani.
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.

Wednesday, 7 February 2018

Emmanuel Okwi akonga nyoyo za mashabiki wa Simba

Emmanuel Okwi akonga nyoyo za mashabiki wa Simba

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Ushindi huo wa Simba unaifanya Azam FC kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 ikiachwa rasmi na Yanga yenye alama 34 katika nafasi ya pili.

Bao pekee lililoipa ushindi Simba limefungwa na nyota Emmanuel Okwi dakika ya 36 na kumfanya mshambuliaji huyo raia wa Uganda kufikisha mabao 13 akiwa juu ya washambuliaji Obrey Chirwa mwenye mabao 10 na John Bocco tisa.

Ushindi wa leo umeifanya Simba ijiongezee alama tatu na kufikisha alama 41 kileleni ikiziacha Yanga yenye alama 34 katika nafasi ya pili na Azam FC yenye alama 33 katika nafas ya tatu.

Msaani Vanessa Mdee atumia million 100 za kitanzania kuiandaa album yake mpya ya Moneymonday

Msaani Vanessa Mdee atumia million 100 za kitanzania kuiandaa album yake mpya ya Moneymonday

Msanii wa muziki, Vanessa Mdee amedai ametumia gharama kubwa katika kuiandaa albamu yake mpya MoneyMonday.

Muimbaji huyo amesema kuwa albamu ya MoneyMonday mpaka kukamilika imemgharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni 100.

“Nimetumia fedha nyingi lakini kwangu sioni tatizo lolote, niliangalia zaidi jinsi gani watu watatambua Vanessa kafika wapi katika kukua kimuziki, fedha hiyo nililipa idara zote kuanzia wasanii walioshiriki matangazo, video nk na bado naendelea kutoa kwa kuwa matangazo bado yanaendelea ,” Vanessa aliuambia mtandao wa Dar 24.

Ameongezea kuwa hajutii matumizi ya kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kuwa lengo lake hasa ni kutoa kazi itakayomwongezea heshima kwenye muziki wake sambamba na kuhakikisha inawifikia watu wa aina zote.

Hivi karibuni Vanesa ameachia albamu yake katika ukumbi wa Mlimani City.

Vanessa ni kati ya wasanii wachache ambao wanajaribu kurudisha utamaduni wa kutengeneza Albamu katika muziki wa Bongo fleva jambo ambalo kwa siku za nyuma limekuwa likififia na kupotea.