Saturday, 30 December 2017

Yajue Madhara ya kutumia Simu ya Smartphone kwenye Giza
    

Yajue Madhara ya kutumia Simu ya Smartphone kwenye Giza     

Mara nyingi watu wengi tuanpenda kutumia simu mahali ambapo pana giza kwa muda mrefu, sisi tunapenda kukuita kukuchati. Kuchati huku nyakati za giza wakati taa imezimwa huwa na madhara yafuatayo.
Kwa sasa, idadi ya wagonjwa kuanzia miaka 30-40 wanatafuta matibabu makubwa. kutokana na matumizi ya simu za mkononi (smart phone) gizani.
Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko singapore amesema: anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.
Hii ni kwasababu wakati wa kutimia simu mahali penye giza huwa tunayalazimisha macho yetu yaweze kuona ya uwezo wake. Na ndo maaana kuna wakati unaweza ukatumia simu muda mrefu mahali penye giza mara baada ya kuacha kutumia simu utaona kama giza limezidi zaidi. Hali hiyo huyafanya macho yako yaanze kurudi katika hali ya ukawaida.
Pia utumiaji wa simu kwenye giza husababisha Kupata saratani ya macho. Hivyo ili uweze kuepuka saratani hivyo ni bora tuache kutumia simu za mikononi gizani ili tujikinge. Simu za mikononi (smartphone) zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani, unabadili mfumo wa seli macho na kupelekea matatizo ya saratani ya macho.
Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi wanazigundua watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo. Hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote hawa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.
Utumiaji wa simu inaweza sababisha na ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.

Madaktari bingwa wa macho 254 kutoka mahosipitalini profesa Li Li atoa hoja kwamba kikubwa cha muhimu ni kwamba ni kuwa mbali na tabia za kutumia simu gizani. Sababu tabia hizi za kutumia simu (smartphone) kabla ya kulala zitakusababishia matatizo ya maisha yako kwa ujumla.
Hivyo ili kujiangalia sisi wenyewe na familia zetu, kwamba hakuna kuzima taa endapo unatumia simu ya mkononi. Wape taarifa haraka wote watumiaji wa simu za mikononi gizani wanaweza kupoteza kwa urahisi sana uwezo wa kuona.

Friday, 29 December 2017

Waziri wa uchukuzi nchini Israel,Yisrael Katz ametaka kuchimbwa kwa reli ya chini kwa chini kwenye mji wa zamani wa Jerusalem

Waziri wa uchukuzi nchini Israel,Yisrael Katz ametaka kuchimbwa kwa reli ya chini kwa chini kwenye mji wa zamani wa Jerusalem

Waziri wa uchukuzi nchini Israel,Yisrael Katz ametaka kuchimbwa kwa reli ya chini kwa chini kwenye mji wa zamani wa Jerusalem karibu na ukuta wa Magharibi na kupewa jina la Donald Trump.

Yisrael Katz alisema kuwa anataka kumpa heshima Rais huyo wa Marekani kufuatia uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Reli hiyo mpya ya chini na kituo cha treni ni sehemu ya mradi wa reli ya mwendo kasi kutoka Tel Aviv inatarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.

Bw. Katz aliliambia gazeti moja la Israel la Yedioth Ahronoth kuwa kuongezwa kwa reli kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem ndio mradi muhimu zaidi kwa wizara ya uchukuzi.

Chanzo: BBC karibu na ukuta wa Magharibi na kupewa jina la Donald Trump.

Yisrael Katz alisema kuwa anataka kumpa heshima Rais huyo wa Marekani kufuatia uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Reli hiyo mpya ya chini na kituo cha treni ni sehemu ya mradi wa reli ya mwendo kasi kutoka Tel Aviv inatarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.

Bw. Katz aliliambia gazeti moja la Israel la Yedioth Ahronoth kuwa kuongezwa kwa reli kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem ndio mradi muhimu zaidi kwa wizara ya uchukuzi.

Chanzo: BBC

SABABU 9 KWA NINI UNYWE MAJI

SABABU 9 KWA NINI UNYWE MAJI

1:Kupunguza uzito: Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari.

2:Afya ya moyo: Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2 au chini ya hapo.

3:Nishati ya mwili: Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama soda, juisi au bia.

4:Tiba ya kichwa: Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja na kuumwa kichwa. Kunywa maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana na kuumwa kichwa mara kwa mara.

5:Ngozi nyororo: Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza safisha ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo.

6:Matatizo ya choo: Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo, kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara.

7:Usafishaji wa mwili: Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.

8:Saratarani: Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa saratani ya kibofu cha mkojo.

9:Mazoezi: Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo. MUNGU akubariki.

Harmorapa amefunguka na kumuomba radhi mtayarishaji mkongwe wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa studio za Mj Records

Harmorapa amefunguka na kumuomba radhi mtayarishaji mkongwe wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa studio za Mj Records

Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kumuomba radhi mtayarishaji mkongwe wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa studio za Mj Records, Master J na kusema kuwa amegundua kuwa alimkosea mkongwe huyo kwenye muziki.
Harmorapa alifunguka hayo alipohojiwa kwenye kipindi cha eNewz cha EATV na kusema katika mwaka 2017 amemkosea sana Master J kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi cha nyuma kupitia kipindi hicho kuwa hamjui wala hamtambua mtayarishaji huyo mkongwe wa bongo fleva. "Nimegundua kuwa nilifanya makosa sana, unajua kipindi kile nasema vile nilikuwa bado sijamjua vizuri Master J hivyo naomba anisamehe tu kwani ulikuwa ugeni katika tasnia hivyo nilikuwa sijamjua vizuri" alisikika Harmorapa.
Harmorapa alishawahi kumkana mtayarishaji huyo kuwa hamfahamu baada ya Master J kunukuliwa akisema kuwa msanii huyo hana kipaji cha muziki na kuimba labda kama atakwenda kufanya vichekesho, jambo ambalo lilionesha kumkwaza Harmorapa.

Pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana

Pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana

DAR: Serikali imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 kuanzia Januari hadi Juni, Pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana
-
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alipozungumza juu ya mwenendo wa uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/18,  changamoto na matarajio na matarajio yake
-
Waziri Mpango pia amesema Serikali imefanikiwa kukusanya wastani wa Sh. trilioni 1.2 kila mwezi baada ya kuziba mianya ya Rushwa na Ufisadi na kuwataka Watanzania kujenga tabia ya kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.

Wolper afunguka mbioni kufunga Ndoa

Wolper afunguka mbioni kufunga Ndoa

Msanii wa filamu Bongo na mwanamitindo, Jacqueline Wolper huenda akafunga ndoa hivi karibuni mara baada ya kuweka wazi mipango yake ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi wake.
Licha ya kutomtaja muhusika, Wolper ameeleza kuwa mpenzi wake huyo ameridhia suala hilo kwani naye pia alikuwa akilihitaji toka mwanzo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper ameandika mengi kuhusiana na hilo ila hapa tumenukuu haya machache;
Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako,umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi, (NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila umemthamini Jacq. Nilipotoka niliteswa sana na mapenzi yaani usaliti, dharau, kukosa na mapenz ya dhati.
Pamoja ya kuwa pia alishatokea mmakonde na kunipeleka mapaka Mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo umefika, umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali nahitaji future husband.
Pia ameongeza kuwa katika mahusiano amejifunza kunyamaza bila kuyaweka hadharani na siku ya leo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Moshi na taratibu nyingine kama mahari kufuata. Wolper afunguka mbioni kufunga Ndoa

Saturday, 16 December 2017