Thursday, 8 February 2018

Hivi ndivyo unavyoweza kujua kama una upungufu wa Maji Mwilini

Hivi ndivyo unavyoweza kujua kama una upungufu wa Maji Mwilini

Upungufu wa maji mwilini ni;
Pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

NINI HUSABABISHA?
Sababu zinazosabababisha mwili kukaukiwa maji huweza kuwa nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni pamoja na:

1. Kuacha kunywa maji
2.Kukaa kwenye joto kwa muda mrefu.
3.Kunywa kiwango kikubwa cha pombe
4.Ungonjwa wa kisukari ambao husababisha mtu kukojoa mara kwa mara.
5. Kutokwa na jasho jingi, kwa sababu ya ama kufanya kazi ngumu au mazoezi.
Hivyo inashauriwa mtu anayetokwa jasho jingi kunywa maji mara kwa mara wakati akiendelea na shughuli inayomtoa jasho.

Kama ukiugua au ukipatwa na homa kali, huweza kupungukiwa na maji mwilini
Kutapika na kuharisha nako huweza kupoteza maji mwilini. Hivyo itakeapo hali hiyo jitahidi kunywa maji mwilini.

Hizi ndizo dalili za kukaukiwa na maji mwilini kwa watoto wadogo;
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

Kukojoa mara chache sana

Mtoto kutokuwa mchangamfu

Macho.

Tumbo au mashavu kubonyea 

Mdomo na ulimi kukauka.

Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.

Dadili za upungufu kwa wazee.
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.

Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Vyakula vinavyoondoa mamumivu wakati wa hedhi kwa wanawake

Vyakula vinavyoondoa mamumivu wakati wa hedhi kwa wanawake

Kila mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika, wapo baadhi ya wanawake huumwa na kiuno, wengine tumbo n.k

Dlili za matatitizo ya hedhi
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

Vifatatavyo ni vyakula vinavyoweza kutibu maumivu wakati wa hedhi

2. Tangawizi
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

2. ufuta.
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

3. Papai
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

4. Juisi za mboga za majani.
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.

Wednesday, 7 February 2018

Emmanuel Okwi akonga nyoyo za mashabiki wa Simba

Emmanuel Okwi akonga nyoyo za mashabiki wa Simba

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Ushindi huo wa Simba unaifanya Azam FC kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 ikiachwa rasmi na Yanga yenye alama 34 katika nafasi ya pili.

Bao pekee lililoipa ushindi Simba limefungwa na nyota Emmanuel Okwi dakika ya 36 na kumfanya mshambuliaji huyo raia wa Uganda kufikisha mabao 13 akiwa juu ya washambuliaji Obrey Chirwa mwenye mabao 10 na John Bocco tisa.

Ushindi wa leo umeifanya Simba ijiongezee alama tatu na kufikisha alama 41 kileleni ikiziacha Yanga yenye alama 34 katika nafasi ya pili na Azam FC yenye alama 33 katika nafas ya tatu.

Msaani Vanessa Mdee atumia million 100 za kitanzania kuiandaa album yake mpya ya Moneymonday

Msaani Vanessa Mdee atumia million 100 za kitanzania kuiandaa album yake mpya ya Moneymonday

Msanii wa muziki, Vanessa Mdee amedai ametumia gharama kubwa katika kuiandaa albamu yake mpya MoneyMonday.

Muimbaji huyo amesema kuwa albamu ya MoneyMonday mpaka kukamilika imemgharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni 100.

“Nimetumia fedha nyingi lakini kwangu sioni tatizo lolote, niliangalia zaidi jinsi gani watu watatambua Vanessa kafika wapi katika kukua kimuziki, fedha hiyo nililipa idara zote kuanzia wasanii walioshiriki matangazo, video nk na bado naendelea kutoa kwa kuwa matangazo bado yanaendelea ,” Vanessa aliuambia mtandao wa Dar 24.

Ameongezea kuwa hajutii matumizi ya kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kuwa lengo lake hasa ni kutoa kazi itakayomwongezea heshima kwenye muziki wake sambamba na kuhakikisha inawifikia watu wa aina zote.

Hivi karibuni Vanesa ameachia albamu yake katika ukumbi wa Mlimani City.

Vanessa ni kati ya wasanii wachache ambao wanajaribu kurudisha utamaduni wa kutengeneza Albamu katika muziki wa Bongo fleva jambo ambalo kwa siku za nyuma limekuwa likififia na kupotea.

Tuesday, 6 February 2018

Mtangazaji wa Clouds Media awahimiza walimu wa kujitolea chuo cha DUCE kutokataa tamaa

Mtangazaji wa Clouds Media awahimiza walimu wa kujitolea chuo cha DUCE kutokataa tamaa


Kufuatia zoezi endelevu la kujitolea kufundisha shule mbalibali za msingi na sekondari wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam linalofanywa na wanafunziwa chuo cha DUCE mnamo tarehe 03 Februari, 2018 wanafunzi hao walikutana na Bw. Harris Kapiga ambae ni mtangazaji wa Clouds Media Group kwa mwaliko maalumu ili kuwatia moyo katika kazi hiyo.

Mkutano huo ulifanyika eneo la Mapinga (Nchi ya Ahadi) Bagamoyo nje kidogo yaJiji la Dar es Salaam ambapo Harris alijitolea kuwa mlezi wao katika shughuli hiyo ya kujitolea kufundisha, huku akiahidi kushirkiana nao katika kutatua changamoto yao ya kupata nauli kuwafikisha katika vituo vya kufundisha.

Katika Makutano hayo Mzungumzaji Harrisi Kapiga aliwatia moyo katika hatua hiyo na kuwaeleza kwa kina sifa na umuhimu wa kujitolea katika kazi.Bw. Kapiga alitaja sifa na umuhimu wa kujitolea kuwa ni pamoja na kukuza ujuzi wa kazi ya utaaluma, kupata ujuzi mpya, kupata marafiki wapya wanaoweza kukuunganisha na fursa za kazi, kujitolea kunaweza kuwa chanzo kizuri cha kazi, kujitolea kunaweza kuwa mwanzo wa kubadili aina ya ujuzi wenye fursa nzuri, lakini pia kujitolea kunaweza kumtambulisha mtu katika jamii na kukubarika.Vilevile Kapiga alieeleza jinsi alivyoguswa na mazungumzo ya mwanzilishi wa zoezi hilo Bw. Cornel na kusisitiza kuwa walimu ni watu muhimu, hivyo amewaasa vijana hao kutokata tamaa maana wao ni watu wa thamani sana.“Nyie ni watu wa thamani sana ni sawa na dhahabu ambayo bado haijasafishwa, ikisafishwa itang’aazaidi”. alisema Harris Kapiga wakati akizungumza katika makutano hayo.Vilevile Dr Isiheko ni mmoja wa wadau waliokuwepo katika makutano hayo ambae pia ni mmiliki wa shule za “Wawetu Elshadai”Dr. Isiheko alisema kuwa kujitolea kunamfanya mtu awe na ujuzi wa ziada katika taaluma yake,hivyo vijana wanatakiwa watafute soko la taaluma zao kwa kujiongeza hasa kujiunganisha na watu wenye fursa.Dr. Isiheko aliongeza kuwa mifumo ya Elimu inatakiwa kujikitakuwafunza vijana namna kuishi bila kutegemea Elimu ya Darasani.

Aidha kwa upande wa wanafunzi hao ambao ni walimu wa kujitolea, Mratibu wa zoezi hilo Bw. Cornel aliiomba serikali kuwapa ushirikiano kwa madai kuwa jambo wanalolifanya ni la kizalendo.Tunaiomba Wizara ya Elimu ipitie mitaala ya mfumo wa elimu ili kuwepo na utolewaji wa Elimu itakayowafanya wanafunzi wa chuo wanapohitimu wawe na uwezo wa kujisimamia bila kutegemea ajira kutoka serikalini na kwingineko, hii itasaidia tatizo la ajira. alisema Bw. Cornel kwa msisitizo.Halikadharika katika hayo yote wanafunzi kadhaa wakiwemo, Sichinga Deo Juma, Sinkama Jacksoni na Petro walipata nafasi kuelezea jinsi wanavyo mfahamu Bw. Harris Kapiga.Wote kwa nyuso za furaha na walieeleza jinsi wanavyovutiwa na uhamasishaji wa Bw. Kapiga hasa kupitia vipindi kama Terminalna Clouds habari vipengere mbalimbali.
Imeeandaliwa kwa usaidizi wa Boniphacezacharia@gmail.com

Monday, 5 February 2018

SHEIKH MKUU MKOA WA DAR: MWISHO WA MANGE MITANDAONI UMEFIKA.

SHEIKH MKUU MKOA WA DAR: MWISHO WA MANGE MITANDAONI UMEFIKA.

Al Haji Mussa Salimu ambae ni Sheikh mkuu, mkoa wa Dar es Salaam ametahadharisha kuwa huu ndo mwaka wa mwisho kwa mwanadada maarufu mitandaoni, Mange Kimambi kutumia mdomo wake kuwatukana watu hasa Viongozi.Akiongea na wanahabari leo Jumatatu Februai 5 2018, amesema kuwa anasikitishwa sana picha zilizopigwa siku ya mazishi ya Sheikh Masoud zinatumika vibaya mitandaoni na mwanadada huyo anayemsadiki kutumika.Amesema wanatumia utaratibu wa kisheria kuwadhibiti wote wanaoandika habari ambazo hazina ukweli huku akiwatuhumu Gazeti la Tanzania Daima kwa chapisho la leo lenye kichwa cha habar, SHEIKH ACHAFUA HALI YAHEWA na baadhi ya vyanzo vingnenchini.“Tutafanya utaratibu wa kisheria kwa wale wote walioingia kichwakichwa kuandika habari ambazo hazima ukweli wakiwamo Jamii forum na magazeti ya Tanzania Daima, nataka wanionyeshe ukweli wa hiyo taarifa”. Amesema Al Haji Mussa.Ameongeza kwa msisitizo kuwa wote wanaotafuta umaarufu kupitia midomo kwa maneno machafu huku akimtaja Mange Kimambi, wacheze na watu wengne na sio viongozi wa dini.“Tunamwambia huyo anayejiita Mange kimambi acheze na watu wengine na sio viongozi wa dini, huu ndio mwaka wa mwisho kwake tutasema na Mwenyezi Mungu na majibu mtayaona”. Amesema Al Haji.
#Darmpya.com

Kufuatia kifo cha Kingunge, CCM yasitisha kampeni kushiriki mazishi

Kufuatia kifo cha Kingunge, CCM yasitisha kampeni kushiriki mazishi

Uongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam umesitisha kampeni za nje kwa siku moja (leo) kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho, Simon Mwakifwamba imeeleza kuwa wanachama, makada na viongozi watashiriki kikamilifu katika msiba huo, hivyo hakutakuwa na kampeni za nje.
Alisema watazingatia ratiba iliyotolewa na msimamizi wa msiba huo Omary Kimbau, hivyo wanaCCM wafike mapema kwa ajili ya kumpumzisha kwenye makazi ya milele komredi Kingunge.

Wachezaji wa Morocco washerehekea baada ya kuifunga Nigeria na kulinyanyua taji la CHAN 2018 nyumbani

Wachezaji wa Morocco washerehekea baada ya kuifunga Nigeria na kulinyanyua taji la CHAN 2018 nyumbani

Michuano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani ( CHAN) imehitimishwa Jumapili kwa ushindi wa wenyeji Morocco waliofanikiwa kulinyanyua taji la michuano hiyo kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nigeria.
Mchezaji wa Morocco Zakaria Hadraf alifanikiwa kupachika wavuni bao la kwanza muda mfupi kabla ya kipindi cha mapumziko huku mchezaji wa Nigeria Peter Eneji Moses akitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano muda mfupi baad ya bao hilo.
Walid El Karti na Hadraf - katika bao lake la pili - waliipatia Morocco uongozi katika mechi hiyo kufikia dakika sitini.
Kampeni hiyo ilikamilishwa kwa bao la Ayoub El Kaabi, aliyegonga chuma mara mbili , na kufanikiwa kulifunga bao lake la tisa katika mashindano hayo ya wachezaji wa nyumbani wa timu za Afrika.
Nafasi ya kwanza ya Morocco ilikuja kunako dakika tatu za mechi wakati Walid El Karti aliposukuma tobwe katika eneo la karibuna lango kuu.
Wenyeji hao walidhani wameshafunga bao lao la kwanza katika dakika ya nne alipoisakata ngozi , kwa bahati mbaya naibu refa akanyanyua bendera akidai kiki hiyo ilisukumwa vibaya kabla ya kumfikia mshambuliaji huyo.
El Kaabi akasukuma hedi na kipa wa Nigeria Oladele Ajiboye ilibidi aokoe matobwe mawili kabla ya shinikizo la Morocco kujipa.
Kwa ukubwa Nigeria ilitegemea pasi ndefu kwa mashambulio yao na Anas Zniti wa Morocco hakuwana kibarua kikubwa kuokoa kabla ya muda wamapumziko.
Dakika mbili baada ya kipindi cha mpumziko Peter Eneji Moses alitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kwa mchezo m'baya dhidi ya Mohammed Nahiri.
Morocco ikaongeza bao la pili kunako dakika sitina wakati kiki ya El Kaabi ilipogonga chuma na kurudi nyuma kumwezesha El Haddad kusukuma kwa mara ya pili tobwe ambalo lilimfanya Ajboye asue sue na kumpa nafasi El Karti kusukuma kwa urahisi hedi ya nguvu ndani ya wavu.
Dakika tatu baadaye Hadraf alilifunga lake la pili baada ya krosi ya El Haddad kumuangukia .
El Kaabi hatimaye alifanikiwa kulisukuma lake kunako dakikda 73 wakati mpira ulipomuangukia mguuni na kumfanya amalize mashindano hayo kama mfungaji bora akiwa amefanikiwa kuyafunga tisa kwa jumla.
Kwa kweli timu ya watu 10 ya Nigeria ilishindwa kuitishia Morocco kabisaa katika nusu ya pili.
Magoli ya El Kaabi huedna yamechangia kummulika mbele ya macho ya koca wa timu ya taifa ya Morocco Herve Renard aliyekuwa anatizama michuano huyo pembeni akitazamia kukamilisha kikosi chake tayari kwa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi.
Siku ya jumamosi Sudani ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Libya penati 4-2 baada ya sare ya bao 1-1.
Katika hatua ya penalti , Sudan ilifanikiwa kufunga penati na kuambulia medali ya shaba katika fainali za CHAN baada ya kuibuka tena nafasi ya tatu walipokuwa waandaaji wa mashindano hayo mwaka 2011, huku Libya wakiibuka mabingwa miaka mitatu baada ya hapo.
Mataifa 16 yalishiriki michuano hiyo ambayo yalipangwa katika makundi manne, ambayo ni Kundi A-wenyeji morocco, Mauritania, Guinea na Sudani, Kundi B-Namibia , Uganda, Zambia na Ivori Coast, Kundi C-Libya Nigeria, Rwanda na Equtorial Guinea.
Kundi D -Lilikuwa na Timu za Congo ,Angola, Cameroon pamoja na Burkina Faso.

HUBERT KAIRUKI KUJENGA KITUO CHA KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA UJAUZITO

HUBERT KAIRUKI KUJENGA KITUO CHA KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA UJAUZITO

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano iliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya muasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH) na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4, 2018. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi na Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu.
Na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG
SHIRIKA la Afya na Elimu la Kairuki limejipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Hubert Kairuki (HKMU), Profesa Salaam, Charles Mgone wakati anazungumzia Maadhimisho ya miaka 19 ya kumbukizi ya marehemu Profesa Hubert Kairuki.
Maadhimisho hayo yameanza Februari 1 mwaka huu na yatamalizika Februari 6 mwaka huu.
Profesa Mgone amefafanua kukumbuku ya maadhimisho jambo kubwa ambalo wamejipanga ni kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.
“Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Hapi,” amesema Profesa Mgone.
Ameongeza kuwa “Kumekuwa na matatizo hasa ya ukosefu wa vituo vya kuwasaidia watu wenye matatizo ya uzazi jambo linalotupa msukumo wa kuanza ujenzi huu”.
Amefafanua kwa sasa wapo katika hatua za mwisho cha kupate kibali kwa ajili ya kuanza ujenzi maana wao wameshajipanga na wameshazalisha wataalamu wa kutosha.
Profesa Mgone amesema kukamilika kwa kituo hicho kitakuwa msaada mkubwa kwani mpaka sasa Hospitali ya Hubert Kairuki imekuwa chachu katika utoaji wa huduma ya afya.
Ameongeza mbali na ujenzi wa kituo hicho wanatarajia kuanzisha kliniki ya mama, baba na mtoto huko Bunju ili kuendeleza kuokoa vifo vya akinamama na watoto hasa waliombali na huduma.
Profesa Mgone amesema jambo lingine wanalolifanya katika maadhimisho hayo ni kutoa huduma za afya bure kwa kipindi cha kuanzia Februari 1-6, 2018 kwenye Hospitali ya Kairuki.
Pia wanajitolea damu kwa hiari ili kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu.
Vile vile wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki watashiriki katika shindano la kujipima ujuzi kuhusu mambo mbalimbali katika taaluma ya afya, maswali ya ufahamu kuhusu Tanzania, maisha ya muasisi marehemu Profesa Kairuki, Jiografia na jamii kiujumla.
“Mwisho wa kilele cha maadhimisho hayo kutafanyika mhadhara wa kitaaluma utakaoendeshwa na Professa Malise Kaisi kuhusu ya mada ‘Maono ya Prof. Hubert Kairuki yanayodumu’ “Pia umuhimu wake katika utoaji wa huduma za afya barani Afrika,” ameeleza Profesa Mgone.
Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) limasimamia Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH) na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN) ambapo muasisi wake ni marehemu Hubert Clement Mwombeki Kairuki aliyezaliwa Juni 24, 1940 Bukoba mkoani Kagera.Mnamo Machi 17, 1987 muasisi huyo alianzisha hospitali ya TAG Mikocheni na mwaka 1992 aliibadilisha jina na kuitwa Mission Mikocheni hospitali ambayo kwa sasa inaitwa Kairuki Hospitali.Mwaka 1997, Prof. Kairuki alianzisha Mikocheni International University na baadae miaka 2 kupita alifariki dunia Februari 6, 1999 na chuo kikabadilishwa kuwa Hubert Kairuki Memorial Univesity.
Wakati hospitali inaanzishwa ilikuwa walikuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa wa nje 200 na wagonjwa wa ndani 30 kwa siku na kwasasa hospitali inauwezo wa kutoa huduma kwayagonjwa wa nje 700 kwa siku na wagonjwa 150 wa ndani ambapo wakati muasisi anafariki chuo kilikuwa na wanafunzi 30 katika fani ya udaktari na uuguzi kwasasa chuo kinatakribani wanafunzi 1509.

Mzee kingunge kuzikwa leo

Mzee kingunge kuzikwa leo

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, shughuli zitafanyika leo
Jumatatu tarehe 5/2/2018 kama ifuatavyo
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili Karimjee Hall kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini Kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani kwa chakula cha jioni
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli nzima
Kingunge Ngombale-Mwiru alifariki Ijumaa wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha baada ya kuumwa na mbwa wake.
Faida za mboga za majani kiafya

Faida za mboga za majani kiafya

Watu wengi tumekuwa hatuna utamaduni wa kula mboga za majani, hii ni kutokana wengi wetu hatujui faida zitikanazo na ulaji mboga hizo. Lakini ukweli ni kwamba ulaji wa mboga za majani ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Na watalaamu mbalimbali wa afya wamethibitisha ya kwamba ulaji wa mboga za majani hasa mboga zenye rangi ya kijani zina umuhimu ukubwa sana latika afya zetu.
Na miongoni mwa faida za ulaji wa mboga za majani ni kama ifuatavyo;
1. Ulaji wa mboga za majani zinapunguza Uwezekano wa Kupata Magonjwa Sugu.
Walaji mboga mboga za kijani wana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa sugu na mara kwa mara kuliko wale wanaokula nyama nyekundu kwa wingi. Endapo utakuwa na utaratibu wa kula mboga za majani mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa wa kuzuia magonjwa yafutayo shinikizo la damu, unene, na utapia mlo.
2. Ulaji wa mboga za majani kwa wingi Ni kinga zuri dhidi ya ugongwa wa kisukari.
Tafiti zilizowahi kufanywa na watalamu wa afya walibaini ya kwamba walaji wa mboga za majani kwa wingi wanauwezekano mkubwa wa kuepuka magonjwa ya kisukuri kwa kiwango kikubwa.
Unachotakiwa kufanya ni kwamba hakikisha mboga za majani ambazo unazitumia zinakuwa katika hali ya ukijani mara baada ya kupikwa. Na wataalamu walikwenda mbali zaidi na kusema mboga ya majani inabidi ipikwe kwa muda wa dakika tano.
Tumia mboga majani wingi kwa manufaa ya afya yako
Faida za kula nanasi

Faida za kula nanasi

Nanasi lina vitamin A, B, C lakini pia lina madini ya chuma, calcium, phosphorus na copper. Pindi mtu atumiapo tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuimarisha mifupa, meno. Misuli na neva za mwili.
Ingawa wapo baadhi ya watu huwa hawapendi kutumia tunda hilin eti kwa madani ya kwamba huwa linawasha kwenye ngozi yam domo mara baada ya kulitumia, inawezekana watu hao wakawa sawa ila ukweli ni kwamba achana na kuwasha kwa mdomo bali wewe angalia faida zitakonazo na tunda hilo.
Zifaatazo ni faida za kula tunda hilo;
1. Husaidia kwa kiwango kikubwa kwa wale wenye matatizo ya choo.
2. Lakini pia inashauriwa ya kwamba kwa wakina mama wajawazito na wale wanyonyeshao walitumie nanasi kwa wingi kwa sababu lina faida lukuki sana.
3. Kwa wale wenye matitizo ya athma pia wanashauriwa walitumie tunda hili kwani lina uwezo wa kutibu ugonjwa huo.
4. Lakini pia miongoni mwa matunda ambayo yana uwezo wa kurudisha kumbukumbu ni tunda hili, hivyo basi kwa wale ambao wana matatizo haya ya kupoteza kumbukumbu wanashauriwa kutumia tunda hili.
5. Lakini pia kwa wale wenye matatizo ya utumbo mwembamba na magonjwa ya koo wanashauriwa watumie tunda hili kwani husaidia sana kutibu magonjwa hayo.
Hivyo basi kila wakati jitahahidi kutumia nanasi kwa faida ambazo nimezieleza hapo juu.