Kufuatia zoezi endelevu la kujitolea kufundisha shule mbalibali za msingi na sekondari wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam linalofanywa na wanafunziwa chuo cha DUCE mnamo tarehe 03 Februari, 2018 wanafunzi hao walikutana na Bw. Harris Kapiga ambae ni mtangazaji wa Clouds Media Group kwa mwaliko maalumu ili kuwatia moyo katika kazi hiyo.
Mkutano huo ulifanyika eneo la Mapinga (Nchi ya Ahadi) Bagamoyo nje kidogo yaJiji la Dar es Salaam ambapo Harris alijitolea kuwa mlezi wao katika shughuli hiyo ya kujitolea kufundisha, huku akiahidi kushirkiana nao katika kutatua changamoto yao ya kupata nauli kuwafikisha katika vituo vya kufundisha.
Katika Makutano hayo Mzungumzaji Harrisi Kapiga aliwatia moyo katika hatua hiyo na kuwaeleza kwa kina sifa na umuhimu wa kujitolea katika kazi.Bw. Kapiga alitaja sifa na umuhimu wa kujitolea kuwa ni pamoja na kukuza ujuzi wa kazi ya utaaluma, kupata ujuzi mpya, kupata marafiki wapya wanaoweza kukuunganisha na fursa za kazi, kujitolea kunaweza kuwa chanzo kizuri cha kazi, kujitolea kunaweza kuwa mwanzo wa kubadili aina ya ujuzi wenye fursa nzuri, lakini pia kujitolea kunaweza kumtambulisha mtu katika jamii na kukubarika.Vilevile Kapiga alieeleza jinsi alivyoguswa na mazungumzo ya mwanzilishi wa zoezi hilo Bw. Cornel na kusisitiza kuwa walimu ni watu muhimu, hivyo amewaasa vijana hao kutokata tamaa maana wao ni watu wa thamani sana.“Nyie ni watu wa thamani sana ni sawa na dhahabu ambayo bado haijasafishwa, ikisafishwa itang’aazaidi”. alisema Harris Kapiga wakati akizungumza katika makutano hayo.Vilevile Dr Isiheko ni mmoja wa wadau waliokuwepo katika makutano hayo ambae pia ni mmiliki wa shule za “Wawetu Elshadai”Dr. Isiheko alisema kuwa kujitolea kunamfanya mtu awe na ujuzi wa ziada katika taaluma yake,hivyo vijana wanatakiwa watafute soko la taaluma zao kwa kujiongeza hasa kujiunganisha na watu wenye fursa.Dr. Isiheko aliongeza kuwa mifumo ya Elimu inatakiwa kujikitakuwafunza vijana namna kuishi bila kutegemea Elimu ya Darasani.
Aidha kwa upande wa wanafunzi hao ambao ni walimu wa kujitolea, Mratibu wa zoezi hilo Bw. Cornel aliiomba serikali kuwapa ushirikiano kwa madai kuwa jambo wanalolifanya ni la kizalendo.Tunaiomba Wizara ya Elimu ipitie mitaala ya mfumo wa elimu ili kuwepo na utolewaji wa Elimu itakayowafanya wanafunzi wa chuo wanapohitimu wawe na uwezo wa kujisimamia bila kutegemea ajira kutoka serikalini na kwingineko, hii itasaidia tatizo la ajira. alisema Bw. Cornel kwa msisitizo.Halikadharika katika hayo yote wanafunzi kadhaa wakiwemo, Sichinga Deo Juma, Sinkama Jacksoni na Petro walipata nafasi kuelezea jinsi wanavyo mfahamu Bw. Harris Kapiga.Wote kwa nyuso za furaha na walieeleza jinsi wanavyovutiwa na uhamasishaji wa Bw. Kapiga hasa kupitia vipindi kama Terminalna Clouds habari vipengere mbalimbali.
Imeeandaliwa kwa usaidizi wa Boniphacezacharia@gmail.com
Imeeandaliwa kwa usaidizi wa Boniphacezacharia@gmail.com
0 comments:
Post a Comment