Friday, 2 February 2018

Diamond Platinumz’, amefunguka na kutoa siri ya kinachowafanya wasanii wote walioko chini ya lebo ya Wasafi (WCB) Kufanikiwa.

SHARE
Msanii wa Bongo fleva na ambaye amepata mafankio makubwa kupitia muziki wake, Naseeb Abdul almaarufu ‘Diamond Platinumz’, amefunguka na kutoa siri ya kinachowafanya wasanii wote walioko chini ya lebo ya Wasafi (WCB), kuwa wanafanikiwa kila wanapotoa wimbo hata kama imechukua muda mchache kuja katika game ya muziki.
Diamond amefunguka hayo siku ya Jumamosi alipokuwa akimkaribisha na kumtambulisha msanii mpya wa WCB, Maromboso ambaye hapo awali alikuwa katika kundi la ‘Ya Moto Band’ kabla kundi hilo halijavunjika na kusambaratika.
Diamond anasema kuwa katika kuwatoa wasanii walio chini ya lebo hiyo, hajawahi kufanya hivyo kama biashara kama wanavyofanya wengine, bali yeye anawatoa wasanii wengine kwa sababu anataka watoke na waweze kusaidiana na kuongeza kuwa wapo wengi wana vipaji lakini wanashindwa kutoka kwa kukosa watu wa kuwasaidia.
Diamond anaongezea na kusema kuwa kinachomtia moyo kutoka kwa wasanii hao ni kwa sababu wamekuwa wakijituma sana na hata kuacha kulala usiku ili kuhakiisha kuwa kazi zao zianakwenda vizuri kwa sababu hawafanyi kwa ajili yake bali ni kwa ajili yao na familia zao.
“Nafikiri kwa sababu mimi sifanya hivyo kibiashara, watu wengi wamekuwa wakiifanya kibiashara lakini mimi ninafanya kwa ajili ya kujikomboa, na kila mtu apate kulingana na kazi ile anayoifanya. Ndio maana kila mtu anaefanya kazi WCB anafanya kazi kwa kujituma na kwa moyo mmoja kwa sababu anajua kabisa kile anachokitengeneza hamtengenezei Diamond au WCB, bali anafanya kwa ajili ya yake na familia yake,” alisema Diamond.
Diamond amekuwa msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye amepata mafanikio makubwa kutokana na muziki wake, jambo lililomuwezesha kutambulika hata katika maeneo mbali mbali ya nje ya nchi pamoja na kufanya kazi na wanamuziki mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Kwa sasa Diamond, pamoja na muziki anajihusisha pia na biashara nyingine kama vile Chibu Perfume, Diamond karanga, na hivi majuzi alitangaza kuanzisha kituo cha runinga na redio cha WCB ambacho pia kitamuwezesha kujiapatia kipato cha kuyaendeleza maisha yake.

SHARE

Author: verified_user

0 comments: