Friday, 2 February 2018

Marekani yaeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa nchini kenya

SHARE
Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya matukio yanayotokea nchini Kenya, ambako kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alijiapisha mwenyewe kuwa ''Rais wa Wananchi'' siku ya Jumanne.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hearther Nauerth amesema malalamiko kuhusiana na uchaghuzi nchini Kenya yanapaswa kusuluhishwa kupitia utaratibu unaofaa wa kisheria.
Ameikosoa pia serikali kwa uamuzi wake wa kuvifungia vituo vitatu vya serikali, ambavyo vilijaribu kurusha matangazo ya moja kwa moja tukio hilo la kujiapisha kwa Raila Odinga.

SHARE

Author: verified_user

0 comments: